Utapambaje chumba cha kulala



Images courtesy of realsimple

Afya njema huenda sambamba na umuhimu wa kulala vizuri/pazuri . Kumbe basi kuna umuhimu wa kupendezesha chumba chako cha kulala kwa kuweka mpangilio mzuri na kupunguza na kulala mahali pasafi na panapopendeza. Katika kukipamba chumba unaweza ukaweka mito na foronya rangi mbalimbali,kuweka maua,kutandika bedcover zilizofumwa au kuweka quilt ukutani kama picha hiyo ya 3,weka picha iliyochorwa kwa rangi ya maji iliyotulivu ukitani,kuweka zuria au mkeka uliofumwa vizuri,kuwa na taa mbili yenye mwanga mkali na isiyokuwa na mwanga mkali.Unaweza ukatengeneza foronya mwenyewe kutokana na mashuka ya maua au kama una kitambaa ukipendacho cha maua au mistari au draft. Swali la udaku: Je unabadili mashuka yako baada ya muda gani?

Mwisho wa Oprah Show...angalia video yake akitangaza.

Image courtesy of Oprah.com
Mwanamke wa shoka atamaliza show yake mwaka 2011. Angalia video toka oprah.com akitangaza kwa masikitiko na habari kamili toka website yake hapa . Kwa kweli vipindi vyake vinaelimisha kama hiki hapa na hapa nilivyowahi kublog huko nyuma. zaidi angalia website yake hapa.Nakutakia weekend njema.

wanaijeria wafika mbali...angalia wanafanya nini!

Waiting for bus by Artist Dilomprizulike DILOMPRIZULIKE
Image courtesy of gasworks

All 4 images ;art by El Anatsui
Above 4 image courtesy of
eatdaily

Ubunifu,ubunifu,ubunifu ni kitu muhimu sana. Wanaijeria hawa Dilomprizulike (habari yake hapa) na Anatsui (habari yake hapa)
sanaa zao zimependwa sehemu nyingi duniani. Anatsui anatengeneza mfano wa kitambaa (picha 2 na ya 4) kutokana na makopo , vifuniko/visoda n.k. Na Dilomplizulike anatengeneza sculptures kutokana na nguo na vitu visivyotumika tena,angalia picha hii ya sanaa yake kutoka universe-in universe
inavyopendeza na kukufanya ufikiri. Picha ya 3 na ya 5 hapo juu ni jinsi anavyounganisha visoda na makopo kutengeneza mfano wa kitambaa. Hii ni changamoto kama una kitu unawaza kutengeneza tengeneza maana huwezi kujua watu watakipenda vipi.Kuna mtu anatengeza sanaa za kuvutia unayemjua? tunaomba jina na sanaa yake.Enjoy!


Fine art Photography....jinsi ya kufanya... na kupata pambo la kipekee.

Viatu na maua madogo niliyoyakata toka maua makubwa ya plastik
mkusanyiko wa vipande vya picha toka magazetini na jarada la kitabu (collage)
mkusanyiko wa vipande vya picha mbalimbali toka magazetini juu jarada la kitabu (Collage) vitu vidogo vidogo nivipendavyo

Maua ya crochet niliyofuma zamani na brooch kwenye kikombe cha mayai

kama hapo juu

kama hapo juu
All Images copyright: sophiesclub

Hata wewe unaweza!La kufanya ni kupanga mpangalio wa vitu vyovyote vile uvipendavyo na kuvipiga picha kutokana na mtizamo wako.Mfano ni hizo picha juu nilizopiga za vitu mbalimbali. Ukisha piga unazikuza na kufrem tayari unapambo la kipekee la nyumbani kwako au zawadi kwa ndugu, jamaa na marafiki au biashara vyovyote upendavyo.Pia usisahau kushare nasi hizo picha.

Fine art photography refers to photographs that are created to fulfill the creative vision of the artist;source wikipedia



Somo linazidi kueleweka TZ...angalia upambaji HomezDeco na Ladyjaydee

Image via homezDeco

Leo nimefurahi kuona blogs mbili wanapromote upambaji na umuhimu wa kuyapenda mazingira yako,somo linazidi kueleweka! Blogs hizo ni homezDeco na ladyjaydee. Nimefurahi kwa kuwa naona wengi tunaanza kuona umuhimu wa kuyapenda mazingira yetu ( kupitia maoni yaliyotolewa). Kwa msisitizo zaidi kama ambavyo huwa nasisitiza ktk blog posts zilizopita, sehemu unayoishi iwe ni nyumba yako au nyumba /chumba cha kupanga ni mahali pako kwa wakati huo na ni reflection yako, ni vema na ni ustaarabu ukipapanga vizuri na kupapendezesha ndani na nje.Sio lazima vitu/mapambo viwe vya gharama bali chagua ulivyo na uwezo navyo na vingine una-recycle na kutengeneza mwenyewe kama ambavyo nimekuwa niblog .Sio tu patakuongezea ufanisi maana kila kitu unajua kilipo bali pia patakupunguzia stress. Tuyapende mazingira yetu kama tunavyojipenda!

Ume-recycle nini mwaka huu?

Postikadi za zamani kuwa kadi za mwaliko
Rula ndefu kuwa ubao wa juu wa meza

Brooch na heleni kuwa magnet

Foronya kutokana na mashati yasiyotumika
All above images courtesy of contryliving

Tupende ku-recycle!kurecycle hakuna mwisho na namna hii tunapata kutumia vitu mbalimbali tulivyonavyo na kuwa na kumbukumbu, kutunza mazingira,kupunguza gharama na kupendezesha sehemu tunazoishi. Je una kitu gani ume-recycle toka mwaka huu uanze? tuambia/tufundishe na sisi tafadhali.Au una kitu unakipenda na unataka kukipatia matumizi mengine ila hujajua ni matumizi gani? Uliza tutafute jibu.

Ubunifu na mpangilio


Images courtesy of elleinterior
Ukichanganya ubunifu na kupenda mpangilio mzuri wa vitu basi itakuwa rahisi kuweka mazingira yako ya ofisi au nyumbani kuwa ya kuvutia. kwa mfano hiyo picha ya pili nimeipenda inaonyesha jinsi mtu huyu anavyopenda mpangilio akaweka droo juu ya nyingine na kupanga vitabu. Ya kwanza unaona jinsi ubunifu wa kufuma kwa krosia ilimradi kupendezesha kitofauti. Gazeti la elleinterior lina mambo mengi mazuri ila maelezo ni kwa kiswid.Haya endeleza ubunifu.

Badili sura ya chumba kwa dakika kumi



images via realsimple
Vitu ulivyonavyo unaweza ukavitumia kwa matumizi mbalimbali tofauti na matumizi yake ya awali (picha ya 2) na pia unaweza tumia mikebe kuwekea vitu mbalimbali,ukipata inayofanana hupendeza zaidi pia kama unasumbuliwa na karatasi kila mahali kama mimi basi tumia hayo makasha ya kuwekea mafaili ofisini kuhifadhia . Namna hii mpangilio wa vitu unakuwa rahisi na kupendeza na kukurahisisha kuona utakachokua unatafuta.

Pamba kwa bei poa

Image courtesy of marthastewartwedding
Mkusanyiko wa makopo yaliyochorwa vizuri nje hupendeza pia kutumika kuwekea maua kama hapa kwenye picha. Unakumbuka makopo yoyote ya kwetu yaliyo na mapambo mazuri nje?Tuambie.Weekend njema na kesho usisahau kuweka ua mezani wakati wa kifungua kinywa harafu nitumie picha.

Sanaa ya aina yake

image cortesy of Arcadia Lyons at flickr
Image courtesy of thedailygreen

Sanaa haina kikomo! Sanaa ya krosia !Enjoy!

Upambaji ni pamoja na mpangilio mzuri wa vitu





All above images courtesy of sampler

Sio mpaka uwe na vitu vya gharama nyumba yako ipendeze,mpangilio mzuri wa vitu hufanya sehemu ipendeze ukiongezea na rangi mbalimbali kwa mfano hicho kitambaa cha draft sehemu inavutia. Angalia picha ya 3,4 na 5 kutoka sampler jinsi vitu vya kawaida kabisa vilivyo pangwa na sehemu inavutia. Inabidi kuwa mbunifu mfano ngazi imetumika kama shelf na kupanga vitu. Miiko kwenye jagi n.k yaani ubunifu wako usiweke kikomo.Namna hii unapata uwazi zaidi na hewa safi na kuwa mfanisi zaidi maana kila kitu unakiona na kukifikia ukikihitaji.enjoy!

Uzuri wetu wa asili tumeupotezea wapi?vipodozi na madhara yake

Image via fashionmanifesto
Mwanamitindo Alek Wek
Image via charcoalink
Lauryn Hill na afro


Image via photobucket
Misuko ya nywele za nyuzi
Image via charcoalink
Mwimbaji Jill Scott na afro la nywele zake
image via fanpics

Uzuri wetu wa asili tumeupotezea wapi?
Sijui tulaumu watengenezaji wa vipodozi vya karne hii au tujilaumu wenyewe kwa kupoteza uzuri wetu wa asili.Aina nyingi za urembo wa karne hii unahatarisha afya zetu ( na za watoto tumboni iwapo mama mjamzito anatumia vipodozi hivi) na pia unatupotezea uzuri wetu wa asili mfano mzuri ni vipodozi vya ngozi na dawa za nywele. Nimekuwa nikifikiri mtu ukimuuliza hivi nywele zako za asili zinafananaje nahisi wengi tumesahau maana tunaweka dawa juu kwa juu. Kuna aina nyingi za kupendeza kama unataka kubadili staili suka mitindo mbalimbali kwa muda mfupi mfupi mradi upumzishe nywele zako kutokana na madhara ya unayoweza kupata kwa kutumia hizi dawa kwa muda mrefu. Sasa basi kabla hujanunua hivi vipodozi vya ngozi,makeups n.k kwa usalama wa afya yako tembelea cosmeticdatabase website ambayo itakuonyesha ni kwa kiasi gani vipodozi hivyo vina madhara. Hizi picha hapo juu nimezipenda sana nikaona nizipost kwakuwa zinawaonyesha hawa akina dada wanavyothamini uzuri wao wa asili.Na kama unavyowaona bado ni wa "kileo" na wenye maendeleo vile vile.Tumia vipodozi vya asili,jali,thamini na jivunie ngozi na nywele zako za asili, ijali afya yako utapendeza zaidi na kujiamini na kwa mtindo huu utakuwa umeyajali mazingira.Enjoy

Leo tuone upambaji wa Wafaransa








all images courtesy of marieclairemaison

Mara nyingi huwa nikiandika napenda kukumbushia kuwa upambaji unakuwa mzuri pale mpambaji anapokuwa creative na kuja na mawazo mapya. Napenda kublog mapambo na upambaji,sanaa n.k kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni ili utakapokuwa unapamba uchanganye ideas za huku na kule na uongezee ujuzi wako hapo utapata matokeo mazuri na tofauti na wapambaji walio wengi. Kama unavyoona ktk picha hizi upambaji wa Wafaransa kutoka 100 idees DECO unaonyesha aina mbalimbali za upambaji wao kama upambaji kwenye kikapu,shells, na upambaji maua ndani ya
mikebe ya vioo yaani maua hayatokezei juu kama kawaida tulivyozoea. Haya jaribu mwenye na pia mfundishe mwenzio.Enjoy

Bluu,zambarau,kijani na wall papers




Images courtesy of skonahem

Natumaini wasomaji wangu nyote wazima kwetu salama!Nimeona upambaji toka Skonahem ( natamani ningejua kusoma lugha yao) wanamapambo mazuri. Picha hizi nimeipenda zaidi kwakuwa nilitaka kuongelea jinsi ambavyo wall papers zinavyopendezesha nyumba/chumba hasa zikiwa ni rangi za kutulia kama bluu,kijani,zambarau. Ila usiweke wallpapers aina moja nyumba nzima zitakuchosha. Weka aina tofauti tofauti vyumba utavyochagua na zenye maua madogo madogo au majani kama hapo juu maana huwa hazichoshi kuziangalia.Enjoy na karibu tena!

Sanaa ya krosia (crochet) - Brazil na Marekani

Images courtesy elainecroche
Sanaa ya krosia imekua sana nchini Brazil wakina mama wanajipatia kipato kwa kufuma vitu mbalimbali. Japo kwetu watu wengi wanaijua sanaa hii tumekuwa hatuikuzi sana na wengi kuishia kufuma vitambaa na sweta za watoto kidogo kidogo. Hatujachelewa kazi kama hizi za mikono zinasoko sana sehemu mbalimbali duniani. Dada huyu wa elainecroche amefuma mkoba mfano wa huo alionao Mwanadada Halle,unaona alivyoufuma vizuri kwa ufundi na kwenye website yake anaonyesha video mbalimbali za kazi zake kama utapenda kujifunza na hapo hapo anauza video hizo na kujiongezea kipato. Ijaribu sanaa hii ni nzuri.Enjoy!

Nifanye biashara gani?-Orodha hii hapa chagua

Image courtesy of boopsie.daisy


Mara nyingi utasikia mtu anasema ...nataka kufanya bishara ila sijui nifanye biashara gani!. Usipate taabu ahbbo wameweka list ndefu hapa ya aina za biashara mbalimbali ambazo mtu anaweza kufanya kuanzia kufundisha computer watoto,uuzaji vitu vya zamani mpaka kuwa proofreader.Pia mysmallbiz nao wana orodha yao hapa na hii ina maelezo zaidi jinsi ya kuanza na imepangwa kwa vipengele .Ipitie upanue mawazo na mpasie mwenzio. Enjoy!

Kina Klothing Yafungua Duka Mtandaoni




All above images courtesy of kinaklothing

Kama usemi wa Mswahili usemavyo "mcheza kwao hutunzwa" haya jipatie mali mpya iliyotulia kazi ya watoto wa nyumbani. Ufuatao ni ujumbe wao kwako na kwa rafiki yako:

"Salaam kwa wadau wote wa blogu ya Absolutely Awesome Things.
Kina Klothing ina furaha kuwafahamisha kuwa tumefungua duka letu mtandaoni na unaweza sasa kununua Tshirt moja kwa moja kupitia http://www.kinaklothing.com/
Kina ni kampuni mpya ya nguo ambayo inawakilisha Bongo na Afrika kwa ujumla. Kwa utambulisho tumetoka na kollektion inayoitwa Uhuru St. kwa sababu neno uhuru linabeba sababu nzima ya sisi kuanzisha Kina.
Vilevile hii ni lebo ya mavazi ya kitaa na Uhuru ni mtaa wa kwanza katika mfululizo wa kollektion zitakazobeba majina ya mitaa mbalimbali ya Bongo na Afrika kwa ujumla.
Kama kauli mbiu yetu inavyosema “Vitu vyetu. Kivyetu” basi ndio tunavyotarajia kuendesha lebo yetu, yaani full uhuru wa kutengeneza kazi zinazotuwakilisha, kwa namna tunayoamua wenyewe.
Tshirt hizi zimesanifiwa mahsusi kwa ajili ya wabongo na marafiki zao ili kuonyesha kuwa wabongo nao tumo katika medani hii ya design; lakini si hivyo tu, ujumbe unaobebwa na nguo kina ni mchango wetu katika harakati za kujenga madaraja kati ya waafrika barani na diaspora kwa kusambaza na kusheherekea yale yanayotuunga pamoja kama waafrika.
Hata hivyo, katika kollektion hii ya kwanza tumeamua “kucheza kwetu” zaidi, tunatumai utatutunza.
Tutembelee http://www.kinaklothing.com/ na tuambie mawazo yako.
Pia usisahau kujiunga nasi katika ukurasa wetu ya facebook (http://www.facebook.com/pages/Kina-Klothing/101720604819) na kutufuatia katika http://www.twitter.com/kinaklothing
Kaa mkao wa kula kwa kollektion inayofuatia, Samora avenue. Iko jikoni.
Amani.
Mkuki na Susan (Kina Klothing)"

Enjoy!

Kazi za mikono




All above images courtesy of babawague
Kazi hizi za mikono za ufinyanzi pendeza kweli kweli,kutoka babawague.com.Enjoy!

Kupamba kwa bei poa



All 3 images courtesy of womansday

Picha hizi zinaonyesha kupamba pasipo kuingia gharama mf. ya kwa kupamba kutumia vyombo ambavyo tayari unavyo,kuweka maua kwenye chupa tupu ulizonazo na kuweka foronya za rangi mbalimbali ambazo unaweza kushona mwenyewe.zaidi angalia womansday.Weekend njema!

Picha za Mfalme wa Pop wakati wa uhai wake


Images courtesy of photos.tmz
Kifo cha Mfalme wa Pop kimetusikitisha wengi wapenzi wa muziki wake,Mungu amlaze salama.Habari za kifo chake hapa,Picha zaidi photos.tmz na salam kutoka watu mashuhuri hapa.

Related Posts with Thumbnails